Van Gaal: Depay na Berghus Kuwakosa Ubelgiji

Kocha mkuu wa Uholanzi Louis Van Gaal ana mashaka kuwa wachezaji wake Memphis Depay na Steven Berghuis watakuwa fiti vya kutosha kwaajili ya mchujo wa Kundi A4 wa ligi ya Mataifa ya Jumapili dhidi ya Ubelgiji.

 

Van Gaal: Depay na Berghus Kuwakosa Ubelgiji

Waholanzi hao waliimarisha nafasi yao kama vinara wa kundi Alhamisi kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Poland, ambapo mabao hayo yalitoka kwa Coady  Gakpo na Steven Bergwijn katika kila kipindi.

Matokeo hayo sasa yanamaanisha kuwa wanatakiwa kutopoteza mchezo wapo unaofuata ambao ni dhidi ya Ubelgiji ili kutinga hatua ya Fainali mwezi Juni. Bergwijn alichukua nafasi ya Teun Koopmeiners aliyejeruhiwa ndani ya dakika tano za mwanzo za mchezo, lakini mshambuliaji huyo baadae akatolewa na kuchukua nafasi Kenneth Taylor, huku Depay akichechemea dakika ya 52 na nafasi yake kuchukuliwa na Vincent Janssen.

 

Van Gaal: Depay na Berghus Kuwakosa Ubelgiji

Van Gaal alikuwa na taarifa njema kuhusu Koopmeiners, lakini Bosi huyo wa Uholanzi hakuwa na matumaini kuhusu nafasi ya Depay na Berghuis kucheza dhidi ya Ubelgiji. “Ninaelewa kwamba Teun tayari alikuwa anahisi nafuu, na nikamchukua Frank De Jong kama tahadhari.  “Sidhani kama Memphis atacheza Jumapili na pia Berghuis. Ni jeraha la mgongo na kwa kawaida huchukua muda mrefu zaidi ya siku chache”

Acha ujumbe