VAR Ilivyomchanganya Arteta

“Sizielewi sheria” -Arteta akibwata baada ya kuchanganywa na sheria za VAR

Teknolojia ya video ya VAR imekuwa ikiwasaidia waamuzi kuhakiki makosa yanayofanywa na wachezaji. Makosa ambayo kwa namna moja au nyingine yanaweza kutoonekana katika mikiki mikiki ya soka dimbani.

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta, alikiri kuwa haelewi au amechanganywa na sheria za VAR baada ya mchezaji wa kikosi chake kutolewa kwa kadi nyekundu.

Eddie Nkeitah alitolewa kwa kadi nyekundu kwenye mechi dhidi ya Leicester City Jumanne. Mechi hii iliisha kwa 1-1.

Huenda Arsenal wangefanya vyema zaidi, lakini haikuwa bahati kwao nyota huyu alitolewa nje wakati wenyeji wakiwa wanaongoza kwa bao 1 dakika ya 75. Dakika 9 mbele Leicester waliweza kurejesha goli.

Mwamuzi Chris Kavanagh alitumia usaidizi wa VAR kabla ya kufanya maamuzi ya kutoa kadi nyekundu.

Staa huyu mwenye miaka 21 alitolewa dimbani kwa kumchezea ovyo mpinzani James Justin,

Bosi huyu wa washika mtutu, ambaye bado alijivunia kikosi chake kwa kazi waliyofanya licha ya kutoa sare, alisema kuwa haelewi sheria lakini hana kitu cha kufanya.

“Sielewi taratibu. Sikumuona muamuzi akiangalia picha yeyote. Lakini siwezi kufanya chochote kwa sasa, ni taratibu.”

Meneja huyu, aliongeza kuwa anajivunia kuwa kikosi chake kilicheza vizuri. Bila kulazimika kucheza wachezaji 10, Arsenal wanaamini bila shaka wangeweza kushinda mechi hii.

49 Komentara

    Arteta labda hakuweza kuzielewa sheria ndomaana alibwata

    Jibu

    Alifanya vizuri sana katika uvumbuzi wake alisaidia uwanjani

    Jibu

    Amepanic Broo ndo ajipange tena#Meridianbettz

    Jibu

    Hii var Ina matamu take na machungu take pia maana kwa wanae shinda kwao ni kicheko sanaa

    Jibu

    Technology ya VAR iko sahihi sana

    Jibu

    Kweli kabisana VAR mdamwingine ionyesha tukio lililofanya kuwa sawa au sio sawa inabidi waamuzi wawe makini . arsenal Jana ingejiweka katika nafasi nzuri ila ndio kwa sababu maamuzi ya mwisho anayo refa uwanjani tu

    Jibu

    Hii VAR inachanganya wengi sana

    Jibu

    VAR ndo ishaamua ye atulie tu ajipange upya

    Jibu

    Makala nzur

    Jibu

    Var ipo sahihi Hakuna tena makerere ya kocha uwanjani aliyebuni amefanya jambo jema

    Jibu

    Muda mwingine inazingua sana

    Jibu

    VAR imekuwa ikiwasaidia waamuzi kuhakiki makosa yanaofanywa na wachezaji

    Jibu

    Some times VAR inachanganya watu wengi

    Jibu

    Asante kwa taalifa

    Jibu

    Ivi hii VAR mbona inazungumziwa Sana inamaana tuamini kwamba inafeli kwenye kutoa maamuzi sahihi.

    Jibu

    Makala nzuri

    Jibu

    Wanted kwa update#meridianbettz

    Jibu

    Bonge la makala

    Jibu

    Duu kuna wakati inamchanganya mtu hi var

    Jibu

    VAR noma

    Jibu

    VAR mda mwingine inazingua sana

    Jibu

    V.A R haiongopi

    Jibu

    Hakuelewa jinsi viongozi wake wanamtaka nn#meridianbett

    Jibu

    Ahsante kwa taarifa

    Jibu

    Haiongopi var

    Jibu

    Kuna muda inachanganya sana unachotegemea sicho

    Jibu

    Anazingua sana muda mwengine#meridianbettz

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Anazingua

    Jibu

    Huenda Arsenal wangefanya vyema zaidi, lakini haikuwa bahati kwao nyota huyu alitolewa nje wakati wenyeji wakiwa wanaongoza kwa bao 1 dakika ya 75. Dakika 9 mbele Leicester waliweza kurejesha goli.# meridianbettz

    Jibu

    Bora tu walivyochanganywa arteta#Meridianbettz

    Jibu

    Kuna mitazamo ya aina mbili tofauti kuhusu VAR.
    Wa Kwanza ni kwamba watu wanakubaliana kwa kauli moja kwamba teknolojia hiyo imekuja na inatenda haki kwenye matukio mbalimbali ambayo hapo kabla yalikuwa siyo rahisi kuonekana na waamuzi.
    Mtazamo wa pili ni kwamba wadau wanadai VAR imekuja kupunguza umakini wa waamuzi uwanjani na wakati mwingine wanafanya maamuzi siyo sahihi kitu ambacho kinapunguzu ladha ya mchezo.
    Tofauti na ilivyokuwa kwenye ligi ya mabingwa ulaya, Bundesliga na La Liga ambao walianza kutumia teknolojia hiyo
    Hadi kufikia sasa kwenye mzunguko wa 12 teknolojia hiyo imeshafanya kazi na kuingia kwenye matukio mengi sana na kutoa uamuzi mbalimbali..
    Katika matukio haya yapo ambayo yalifanyiwa uamuzi ambao ni sahihi na baadhi yaliotolewa uamuzi ambao umeonesha kuna utata.
    Manchester City 2-2 Tottenham Hotspurs
    Mechi hii ilikuwa ni kwenye mzunguko wa pili ambapo ndani ya dimba la Etihad, Man Cirty walikuwa wakiwakaribisha Tottenham Hotspurs. Hiyo ilikuwa ni Agosti 17.
    Baada ya piga nikupige timu hizo zilifika kwenye dakika za majeruhi matokeo yakiwa ni 2-2. Kwenye sekunde za mwisho kabisa Man City walihisi kunyakuwa alama zote tatu baada ya Gabriel Jesus kuukwamisha mpira wavuni.
    Wakati wachezaji wa Man City pamoja na watu wao wa benchi la ufundi sambamba na mashabiki wakiwa kwenye dimbwi zito la furaha ndipo mwamuzi Michael Oliver alitonywa kuhusu tukio fulani kabla ya bao kufungwa.
    Mwamuzi aliambiwa kuwa Aymeric Laporte ambaye ni mlinzi wa Man City aliunawa mpira kabla ya kufika kwa mfungaji na hivyo baada ya kuhakikishiwa kuhusu suala hilo alilifuta bao hilo na mechi ikaisha kwa 2-2.
    Hilo ndiyo lilikuwa tukio la kwanza kubwa zaidi la kusisimua msimu huu ambapo mashabiki wa soka la Uingereza walianza kulishuhudia.
    Hata hivyo kwenye tukio hilo uamuzi ulikuwa ni sahihi hasa ukizingatia sheria mpya za kuunawa mpira ndani ya boksi.
    Arsenal 2-2 Crystal Palace
    Mechi ya Novemba 2 ambapo Arsenal walikuwa nyumbani kuilika Crystal Palace. Kwenye wiki hii naweza kusema kuwa EPL ilishuhudia matukio mengi sana yakiamuliwa na VAR.
    Ndani ya mechi hii tu Crystal Palace walizawadiwa penati ambayo ilitokana na VAR. Lakini tukio kubwa zaidi ilikuwa ni kwenye dakika za majeruhi ambapo mlinzi wa Arsenal, Sokratis Papastathipoulos alidhani kuwa amefanikiwa kuipa timu yake bao la tatu na ushindi kwenye mchezo huo.
    Bao hilo alifunga kwa kichwa na baada ya kushangilia kwa muda mrefu mwamuzi alilifuta bao hilo kwa madai kuwa mchezaji wa Arsenal, Collum Chambers alimfanyia madhambi Gary Cahil wa Palace kabla ya kufungwa kwa bao hilo hivyo bao likafutwa na mechi ikaisha 2-2.
    Maamuzi hayo yalikuwa na utata hasa ukiangalia kwa umakini madhambi aliyochezewa Cahil dhidi ya Chambers
    Lakin kwa tukio la jana me nko pamoja na kocha wangu arterta kiukwel ukiangalia inapoteza sana muda

    Jibu

    VAR hikopoa sana aiwezi kuongopa arteta atulie tu acvurugike

    Jibu

    var bhana kuna mda inasaidia na kuna mda inaumiza

    Jibu

    VAR siku zote unasema Kweli

    Jibu

    VAR hipo sahh inatenda HAKI

    Jibu

    VAR ni nzuri sana lakini inaboa

    Jibu

    Arteta asichanganyikiwe kikubwa ni kujiweka sawa na kikosi chake mamb mengine yaendelee

    Jibu

    VAR hatariii

    Jibu

    Mechi ilijua na umuhimu kwake ndo maana

    Jibu

    Arteta asiwe kama si muelewa VAR ni teknolojia ili leta mapinduz kwenye mpira wa miguu kwa sabab kuna makosa mengi si refalii akayaona kwa macho mpka kifaa maalum

    Jibu

    Asanten kwa tarifa.

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Maoni:VAR inazingua noyooo

    Jibu

    Muda mwingine Hina xingua sana

    Jibu

    Arteta awaulize vizuri Liverpool matumzi ya VAR wanafahamu vizuri faida zake

    Jibu

    VAR iko vizuri.

    Jibu

    VAR inalalamikiwa sana kwamba haiko sahihi ila ili linatokea sana kwa wanao poteza mechi.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.