VAR Kuendelea Kutimika Uingereza 2024/25

Usaidizi wa picha za video maarufu kama VAR kuendelea kutimika katika ligi kuu ya Uingereza kwa msimu wa 2024/25 baada ya timu 19 kati ya 20 kupiga kuea ya ndio kwa matumizi ya VAR.

Kulikua na taarifa huenda VAR isitumike msimu ujao kwenye ligi kuu ya Uingereza na ndio sababu ya kupigiwa kura ili kuamua hatma yake, Lakini timu 19 zimekubali zinazoshiriki ligi kuu ya Uingereza kasoro klabu ya Wolves tu.UINGEREZAKumekua na malalamiko mengi kuhusiana na VAR kwenye ligi hiyo pendwa kabisa ulimwenguni, Jambo ambalo lilifanya mamlaka inayosimamia ligi kutaka timu zinazoshiriki ligi hiyo zenyewe zichague kua zitaendelea na mfumo huo au utaondolewa.

Ni wazi msimu ujao utaratibu huo utaendelea kwani timu 19 zimekubali kuendelea na matumizi ya VAR wakipiga kura za ndio, Huku klabu pekee ambayo imeonekana kuleta pingamizi ilikua ni Wolves lakii mwisho wa siku kura yao haina nguvu kwakua timu zingine zote zimekubali.UINGEREZAPamoja na kubaki kwa VAR ambayo imekua ikisababisha malalamiko mengi sana kwenye ligi kuu ya Uingereza, Lakini timu zitahitaji maboresho na umakini mkubwa ili kupunguza makosa ambayo yamekua yakifanyika na waamuzi ambao wanakua wanaziongoza VAR.

Acha ujumbe