Beki wa klabu ya Manchester United Harry Maguire pamoja na kiungo mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Jack Grealish wameachwa kwenye kikosi cha Uingereza ambazo kitashiriki michuano ya Euro 2024.
Beki Maguire yeye anakosekana kwenye kikosi cha mwisho cha wachezaji 26 kutokana na majeraha ya misuli ambayo aliipata klabuni na madaktari wamethibitisha bado hajapona hivo hatokua tayari.Kiungo Jack Grealish yeye yupo sawa bila majeraha yeyote na sababu ya kutokuepo kwenye kikosi cha mwisho kitakachsafiri kuelekea nchini Ujerumani kwenye michuano ni kua hatoshi na waliobaki wameonesha ubora zaidi yake.
Beki Harry Maguire ameeleza masikitiko yake kupitia mitandao yake ya kijamii juu kukosa michuano ya Euro mwaka 2024, Kwani anaeleza alipambana kwa kiwango kikubwa ili kurejea uwanjani mapema aweze kushiriki Euro lakini haikuwezekana.Kikosi kamili cha Uingereza kitakachoshiriki michuano ya Euro 2024 kinatarajiwa kuwekwa wazi usiku huu au kesho, Huku mpaka sasa wachezaji waliopunguzwa ni beki huyo wa Man United, Jack Grealish, James Maddison, Curtis Jones, Jarrel Quansah wachezaji wanatakiwa wabaki 26 kwajili ya michuano ya Euro mwaka itakayopigwa kule nchini Ujerumani.