Ac Milan Mawindoni kwa Nyota wa Bologna

Klabu ya Ac Milan imeanza maboresho kuelekea msimu ujao na sasa inawinda saini ya winga matata wa klabu ya Bologna Joshua Zirzkee raia wa kimataifa wa Uholanzi.

Ac Milan baada ya kuachana na kocha Stefano Pioli wameonekana kua makini na kuhitaji kurejesha ushindani mkubwa katika ligi kuu ya Italia na ulaya kwa ujumla na baada ya kumalizana na kocha mpya Joshua Zirzkee ndo amekua chaguo la kwanza kwa klabu hiyo.ac milanKlabu hiyo imekua haina msimu mzuri sana ndani ya ligi kuu ya Italia msimu uliomalizika na hata ulaya kwani walitokea kwenye hatua ya makundi, Hivo mabosi wa klabu hiyo wakaamua kuachana na kocha Stefano Pioli na kumleta Paulo Fonseca ili kuanza mapinduzi na mabadiliko klabuni hapo.

Mpaka sasa klabu hiyo ipo kwenye hatua nzuri na uongozi wa mchezaji Joshua Zirzkee na klabu hiyo imeieleza klabu ya Bologna kua wako tayari kulipa kiasi cha €40 Milioni ambapo mkataba wa mchezaji huyo ndivyo unaeleza kua klabu itakayoweza kulipa kiasi hichi inampata mchezaji.ac milanKwa upande wa mchezaji Joshua Zirzkee inaelezwa yeye yuko kwenye hatua za mwisho za kukubaliana maslahi binafsi na klabu ya Ac Milan, Lakini pia vilevile anavutiwa na mpango wa mbeleni wa klabu hiyo bila kusahau anafurahia maisha ndani ya Italia.

Acha ujumbe