Kikosi cha Uingereza Euro 2024 Hadharani

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza na benchi lake la ufundi wamekileta hadgarani kikosi cha timu hiyo ambacho kitakwenda kushiriki michuano ya Euro mwaka 2024 nchini Ujerumani.

Uingereza waliita kikosi cha wachezaji 33 ambacho kilikua kikosi cha awali wakitarajia kupunguza wachezaji saba ili kusalia wachezaji 26 tu ambao watasafiri kuelekea nchini Ujerumani kuliwakilisha taifa hilo.UingerezaWachezaji 26 ambao wamebaki kwenye kikosi ni kama wafuatao Magolikipa Jordan Pickford, Aaron Ramsdale, Dean Henderson, Mabeki, Kylie Walker, Kieran Trippier, Marc Guehi, Lewis Dunk, Joe Gomez, John Stones, Ezri Konsa, Luke Shaw Viungo, Conor Gallagher, Trent Alexender Arnold, Kobbie Mainoo,Declan Rice, Adam Wharton Washambuliaji, Jude Bellingham, Jarrod Bowen, Ollie Watkins, Cole Palmer, Eberechi Eze, Harry Kane, Ivan Toney, Anthony Gordon, Bukayo Saka, pamoja na Phil Foden.

Wachezaji 7  waliotemwa kwenye kikosi hicho ambao waliitwa kwenye kikosi cha awali cha wachezaji 33 ni pamoja na James Maddison, Jack Grealish, Curtis Jones, Jarrad Branthwaite, Harry Maguire, James Trafford, na Jarrel Quansah.UingerezaKikosi cha timu ya taifa ya Uingereza ni moja ya mataifa ambayo yanapewa nafasi kubwa ya kutwaa  ubingwa kwenye michuano ya Euro 2024, Kwani ni moja ya timu iliyo na vipaji vingi maridhawa kikosini lakini pia inakumbukwa kwenye michuano iliyopita timu hiyo ilicheza fainali na kupoteza kwa changamoto ya mikwaju ya penati mbele ya timu ya taifa ya Italia.

Acha ujumbe