Toni Kroos Kufanya Kazi Akademi ya Madrid

Aliyekua kiungo wa klabu ya Real Madrid Toni Kroos anatarajiwa kufanya kazi na timu ya vijana ya klabu hiyo (Akademi) punde tu baada ya kutangaza kustaafu soka mwishoni mwa mwezi ulioisha.

Toni Kroos alitangaza kuachana na soka na michuano yake ya mwisho itakua Euro 2024 ambapo timu yake ya taifa ya Ujerumani ndio watakua wenyeji wa michuano hiyo mwaka huu.toni kroosBaada ya kutangaza kustaafu ikiaminika ataenda kuwekaza nguvu kwenye akademi yake zaidi, Lakini taarifa zimetoka kua mchezaji huyo atafanya kazi kwenye akademi ya Real Madrid hivo ni wazi atakua anafanya kazi kwenye akademi zote mbili.

Kiungo huyo ambaye ameondoka klabuni hapo kwa heshima kubwa akiwa ameshinda taji la ligi ya mabingwa ulaya na ligi kuu ya Hispania, Huku akitarajiwa kurejea klabuni hapo kufanya kazi tena lakini awamu hii hataitumikia klabu kama mchezaji.toni kroosKiungo Toni Kroos baada ya michuano ya Euro 2024 kumalizika ni rasmi atakua ametundika daluga, Lakini haitakua amechana na mpira moja kwa moja kwani atarejea ndani ya klabu ya Real Madrid na kufanya kazi kwenye akademi ya klabu hiyo.

Acha ujumbe