Toni Kroos Kuongeza Mkataba Madrid Mpaka 2025

Kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ujerumani Toni Kroos inaelezwa yuko kwenye hatua za mwisho za kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka Juni mwaka 2025.

Toni Kroos mkataba wake wasasa unamalizika mwishoni mwa msimu huu klabu ya Real Madrid imerudi mezani na kiungo huyo na kufanikiwa kumshawishi asaini mkataba mpya ambao utaendelea kumuweka klabuni hapo mpaka 2025.toni kroosKlabu ya Real Madrid imekua na utaratibu wa kuongeza mwaka mmoja mmoja kwa kila mchezaji ambaye amevuka miaka 30 klabuni hapo, Kwani msimu uliomalizika mchezaji huyo aliongeza mkataba wa mwaka mmoja na pacha wake wa muda mrefu kwenye eneo la kiungo klabuni hapo Luca Modric.

Kiungo huyo ameeendelea kua na kiwango bora jambo ambalo limewashawishi viongozi wa klabu hiyo na kuamua kufikia uamuzi wa kumuongezea mkataba mwingine wa mwaka mmoja aendelea kusalia ndani ya viunga vya Santiago Bernabeu.toni kroosTaarifa hizi zimekuja siku chache baada ya kiungo huyo kuendeleza makali yake kwenye timu ya taifa ya Ujerumani ambapo amerejea baada ya kustaafu mwaka 2021, Toni Kroos anaendelea kubaki kama chaguo la kwanza kwenye eneo la katikati ndani ya klabu ya Real Madrid.

Acha ujumbe