Jamie Vardy Aongeza Mkataba Leicester City

Mshambuiliaji wa klabu ya Leicester City Jamie Vardy ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo mpaka mwaka 2025 baada ya klabu hiyo kurejea ligi kuu ya Uingereza.

Klabu ya Leicester City ilishuka daraja msimu wa 2022/23 na moja ya wachezaji waliokubali kushuka daraja na klabu hiyo ni pamoja na Jamie Vardy ambaye pia amefanikiwa kuirejesha klabu hiyo ligi kuu ya Uingereza.jamie vardyLeicester City itakua moja ya timu zitakazocheza ligi kuu ya Uingereza mwaka 2024/25, Huku mshambuliaji huyo akiwa moja ya wachezaji waliofanya kazi kubwa kuirudisha klabu hiyo kwenye ligi kuu ya Uingereza msimu ujao.

Klabu hiyo ni kama inaonekana kulipa fadhila kwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, Kwani ni wachezaji wachache sana ambao hukubali kushuka daraja na timu lakini staa huyo alikubali kushuka daraja na timu na hatimae kaipambania mpaka imepanda tena.jamie vardyMshambuliaji Jamie Vardy amekua moja ya wachezaji tegemezi sana ndani ya klabu ya Leicester City kwa takribani misimu tisa sasa, Hivo kuongezewa kwake mkataba mwingine wa mwaka mmoja inaonesha bado klabu hiyo inathamini mchango wa gwiji huyo klabuni hapo.

Acha ujumbe