Messi: Real Madrid ni Timu Bora Duniani

Staa wa zamani wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amefanya mazungumzo na chombo kimoja cha habari nchini kwao Argentina na kuzungumza kua klabu ya Real Madrid ni bora duniani.

Lionel Messi amezungumza hayo kutokana na klabu ya Real Madrid kushinda taji la ligi ya mabingwa ulaya wikiendi iliyomalizika, Jambo ambalo limemfanya gwiji kuipa maua yake klabu ya Real Madrid.messiMshindi huyo wa kombe la dunia 2022 hakuishia hapo kwani alisema kwa maana ya matokeo kweli Real Madrid, Lakini kwa namna ya uwezo na kucheza mpira anaamini Manchester City ni klabu bora duniani.

Mpaka sasa staa huyo amewachanganya mashabiki wa mpira kwani ametaja timu mbili duniani ambazo Real Madrid na klabu ya Manchester City huku wakiamini hajapenda kuizungumza Madrid ila imekua hakuna namna.messiLakini pia kwa upande wa mashabiki wa klabu ya Barcelona wenyewe kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii wameonesha kutokufurahishwa na kilichofanywa na Messi kuisifia klabu ya Real Madrid.

 

Acha ujumbe