BAADA ya Jana Klabu ya Azam FC kutangaza kumsajili mshambuliaji wao wa zamani Adam Adam Kwa mkataba wa mwaka mmoja Baada ya kumaliza mkataba wake na Mashujaa FC.
Imefahamika kuwa uongozi huo Umepanga kuwarejesha kikosini mwao waliokuwa wachezaji wao wanne au zaidi Kwa ajili ya matumizi ya Msimu Ujao ambao watakwenda Ligi ya Mabingwa Afrika.Miongoni mwa wachezaji hao lipo jina la Farid Mussa ambaye mkataba wake ndani ya Yanga umetamatika na hakukuwa na mazungumzo mapya yankuongeza mkataba mpya na amekuwa na changamoto ya kupata nafasi ya kucheza hasa msimu huu.
Nyanda Aishi Manula naye yupo kwenye mipango yao na ikimbukwe anatumikia mkataba ndani ya Simba licha ya yeye mwenyewe kuridhia kurejea ndani ya klabu ya Azam Fc na kilichosalia ninmazungumzo ya kuvunja mkataba na yeye kubeba mabegi yake na kurejea Chamazi.
Shaban Chilunda kwasasa ni mchezaji huru baada ya mkataba wake na waliokuwa waajiri wake Simba kuisha, ingawa huyu yeye uwezekano wake wa kurejea Azam ni mdogo zaidi licha ya kuwa ni mchezaji kipenzi Cha Bosi wa timu hiyo, kutokana na mdororo wa kiwango chake.Zipo taarifa za kikachero ambazo Meridian Sports zimenasa pia kuwahusu Salumu Abubakary ‘Sure Boy’, Shomari Kapombe, John Bocco na Erasto Nyoni.
Kapombe na Sure Boy Wanakwenda kucheza, lakini Bocco na Nyoni ni Kwa ajili ya utendaji na timu za vijana.