Ac Milan Yamchukua Kocha wa Lille

Klabu ya Ac Milan inaelezwa kumalizana na aliyekua kocha wa klabu ya Lille ya nchini Ufaransa Paulo Fonseca akitarajiwa kutangazwa siku za usoni ndani ya klabu hiyo.

Ac Milan iliachana na kocha wake Stefano Pioli ambaye amedumu klabuni hapo kwa muda kidogo na kufanikiwa kuwapa taji la ligi kuu ya Italia, Huku wakimchukua kocha huyo wa klabu ya Lille.ac milanPaulo Fonseca amekua moja ya makocha waliofanya vizuri ndani ya ligi kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1, Hivo wababe hao wa soka nchini Italia wakiamua kumchukua kuziba nafasi ya kocha Stefano Pioli.

Mabingwa hao wa Italia misimu miwili iliyopita hawakua na msimu mzuri sana mwaka 2023/24 jambo ambalo liliwafanya viongozi wa klabu hiyo kuamua kuachana na kocha Stefano Pioli.ac milanMsimu wa mwaka 2024/25 kocha Paulo Fonseca atakua na kazi ya kuijenga Ac Milan ambayo italeta ushindani kwenye ligi kuu ya Italia pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa ulaya ambayo hawakufanya vizuri pia msimu uliomalizika.

Acha ujumbe