Maguire Apindua Meza Kibabe

Beki wa klabu ya Manchester United Harry Maguire amepindua meza kibabe baada ya kutangazwa kua mchezaji bora wa mwezi kunako ligi kuu ya Uingereza kwa mwezi Novemba.

Maguire amepindua meza kwani miezi kadhaa nyuma alikua mchezaji aliyeonekana hafai na kuzomewa na mashabiki wa klabu yake, Lakini siku za hivi karibuni ameonekana kurejesha makali yake na kuanza kuimbwa tena.maguireBeki huyo wa kimataifa wa Uingereza amekua na kiwango bora tangu apate nafasi ya kuanza tena ndani ya klabu hiyo, Kwani aliiongoza Man United kupata alama tisa kwenye michezo mitatu ya mwezi Novemba.

Kiwango alichokionesha ndani ya mwezi Novemba akiwa kama beki ambaye aliongoza safu ya ulinzi klabuni hapo, Klabu hiyo ilipata alama tisa katika michezo mitatu na kutokuruhusu goli lolote mwezi Novemba.maguireBaada ya kiwango hicho ndipo beki Harry Maguire kutangazwa kama mchezaji bora wa mwezi wa ligi kuu ya Uingereza akifanikiwa kuwashinda wapinzani wake, Hii imefanya beki huyo kusifiwa sana kutokana na namna alivyorejea kwenye ubora wake baada ya kukosolewa kwa muda mrefu.

Acha ujumbe