Manchester United Yatamba Novemba Epl

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kutawala tuzo za ligi kuu ya Uingereza ambapo wamefanikiwa kuchukua tuzo tatu katika ligi hiyo kwa mwezi Novemba.

Manchester United imetwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ambapo mshindi ni Harry Maguire, Tuzo ya kocha bora wa mwezi amechukua kocha Erik Ten Hag, Huku Alejandro Garnacho akichukua tuzo ya goli bora la mwezi.manchester unitedHarry Maguire amechukua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kutokana na ubora mkubwa aliouonesha katika michezo mitatu aliyocheza mwezi Novemba, Huku akiisaidia klabu hiyo kukusanya alama zote tatu na kutokuruhusu goli katika mwezi husika.

Kocha Erik Ten Hag kwa upande wake alifanikiwa kuiongoza klabu hiyo kukusanya alama zote tisa katika michezo mitatu waliyocheza mwezi Novemba akiwazidi makocha wote ndani ya mwezi huo kwakua hakuna aliyekusanya alama tisa.manchester unitedWinga wa klabu ya Manchester United Alejandro Garnacho amefanikiwa kutwaa tuzo ya goli bora la mwezi baada ya kufunga goli la tiktak dhidi ya klabu ya Everton, Huku Man United wakishinda kwa mabao matatu kwa bila ni wazi klabu hiyo imefanikiwa kuutawala mwezi Novemba katika ligi kuu ya Uingereza.

Acha ujumbe