Kocha wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti ameweka wazi viungo wake wawili Aurelien Tchouameni na Arda Guler wako mbioni kurejea ndani ya klabu hiyo.
Kocha Ancelotti amezungumza na wanahabari leo kuelekea mchezo wao wa kesho wa ligi kuu ya Hispania dhidi ya Real Betis, Ndipo aliweka wazi kua viungo wake wawili hao ambao wanasumbuliwa na majeraha wako mbioni kurejea dimbani.Viungo Aurelien Tchouameni na Arda Guler walikua wanasumbuliwa na majeraha kwa kipindi cha mwezi mmoja nyuma, Lakini baada ya taarifa ya kocha huyo ni wazi kua wachezaji hao wanaendelea vizuri na wako mbioni kurejea.
Kiungo Tchouameni alikua nguzo muhimu ndani ya klabu ya Real Madrid kabla ya kuumia, Huku mchezaji Arda Guler yeye akiwa bado hajafanikiwa kucheza mchezo hata mmoja klabuni hapo tangu ajiunge akitokea klabu ya Fenerbahce ya nchini Uturuki.Baada ya kueleza urejeo wa Tchouameni na Arda Guler kocha Ancelotti ameweka wazi kua wachezaji wengine muhimu klabuni hapo wanaoandamwa na majeraha Vinicius Jr na Eduardo Camavinga watarejea mwaka 2024.