Beki wa klabu ya Manchester United Victor Lindelof inaelezwa atakosekana katika mchezo wa kesho wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya klabu ya Bournamouth katika dimba la Old Trafford.
Kocha Erik Ten Hag ameweka wazi leo katika mkutano wa waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho, Huku akisema Victor Lindelof ataukosa mchezo wa kesho na beki Raphael Varane atakuepo kwenye mchezo wa kesho.Victor Lindelof alitolewa mapumziko katika mchezo dhidi ya Chelsea ambao Manchester United walipata ushindi wa mabao mawili kwa moja, Katika mchezo huu haikuwekwa wazi kua mchezo huo ndio aliumia beki huyo lakini mpaka sasa inaelezwa ndipo beki huyo alipata majeraha yake.
Baada ya taarifa za kuumia beki huyo wa kimataifa wa Sweeden lakini taarifa njema ni za urejeo wa beki Raphael Varane ambaye alikosekana katika mchezo uliomalizika dhidi ya klabu ya Chelsea.Taarifa kutoka ndani ya Manchester United bado hazijaeleza kua beki Victor Lindelof atakosekana kiwanjani kwa muda gani, Baada ya kuumia kwa beki huyo ni muendelezo wa wimbi la majeraha ambayo yanaiandama klabu hiyo msimu huu.