KIGOGO GEITA GOLD AWEKWA KANDO

Menejimenti ya Klabu ya Geita Gold imefanya mabadiliko ya kiutendaji katika nafasi ya Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo iliyokuwa inatumikiwa na Bwana Saimon Joseph Shija ambapo amepangiwa majukumu mengine

Nafasi hiyo kwa sasa itakaimiwa na majukumu yote ya kiutendaji yataratibiwa na Katibu msaidizi wa Klabu hiyo Bwana Ramadhan Bukambu, hadi pale klabu itakapoamua maamuzi mengine

Saimon Shija, amehudumu katika nafasi hiyo ya Mtendaji Mkuu wa klabu ya Geita Gold Fc tangu mnamo mwaka 2021 kabla ya kutenguliwa katika nafasi yake hiyo.

Acha ujumbe