Kiungo wa klabu ya Tottenham Hotspurs James Maddison ametemwa kwenye kikosi cha mwisho cha Uingereza ambacho kinatarajiwa kushiriki michuano ya Euro 2024 nchini Ujerumani.
Maddison alikua kwenye kikosi cha awali cha Uingereza ambacho kilikua na wachezaji 33, Lakini kocha Gareth Southgate amemtema mchezaji huyo kwenye kikosi chake kitakachoelekea Ujerumani kushiriki Euro 2024.Kiungo huyo ameondoka kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uingereza usiku wa jana ikiwa imeshabainika kua hatakua sehemu ya wachezaji 26 wa mwisho ambao wataiwakilisha Uingereza kwenye michuano ya Euro.
Wachezaji wataendelea kupunguzwa taratibu kuelekea ndani ya wiki hii ili kupata orodha kamili ya wachezaji ambao wataiwakilisha Uingereza kwenye michuano ya Euro, Huku kiungo huyo wa Tottenham akiwa miongoni mwa wachezaji wa mwanzoni kukatwa.Wachezaji wanaotakiwa kupunguzwa ili kubaki idadi ya wachezaji 26 kutoka 33 ni wachezaji 7, Hivo baada ya kiungo James Maddison kupunguzwa ni wazi wachezaji wengine sita wataungana nae ili kutimiza idadi ya wachezaji wanaotakiwa kuiwakilisha Uingereza kwenye michuano ya Euro 2024.