Pepe Kutimka Porto Huru

Beki kisiki mkongwe raia wa kimataifa wa Ureno Pepe Lima anatarajiwa kuondoka klabuni hapo kwa huru kuelekea msimu ujao na hiyo ni baada ya kuondoka kwa kocha wa klabu hiyo Sergio Conceincao.

Pepe anakamilisha taratibu za mwisho na klabu hiyo ili kuangalia malisho klabu nyingine ambayo atakubaliana nayo siku za mbeleni, Lakini ni wazi beki huyo anatimka ndani ya Porto.PepeBeki huyo ameitumikia klabu ya Fc Porto kwa misimu mitano sasa tangu mwaka 2019 arejee klabuni hapo akitokea Besiktas ya Uturuki, Huku akifanikiwa kwa kucheza kwa kiwnago bora kabisa licha ya umri wake.

Beki huyo mkongwe mwenye umri wa miaka (41) bado anaonekana kua na mvuto sokoni licha ya umri wake kua mkubwa, Kwani ameonesha ubora mkubwa sana kwa miaka mitano ambayo ameitumikia klabu ya Fc Porto.PepeMpaka sasa haijafahamika Pepe Lima atatimkia klabu gani huenda ikawa ndani ya bara ulaya au akaelekea alipo rafiki yake wa muda mrefu Cristiano Ronaldo kunako ligi kuu ya Saudia Arabia ambayo kwasasa imekua kivutio cha wachezaji wengi.

Acha ujumbe