Klabu ya Bayern Munich ipo kwenye mkakati wa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Uholanzi Xavi Simons ambaye ni mchezaji wa PSG anayekipiga kwa mkopo klabu ya Rb Leipzig.
Bayern Munich inaelezwa ipo kwenye mkakati wa kumpata kwa mkopo mchezaji huyo, Kwani klabu yake ya PSG haina mpango wa kumuuza kwasasa jambo ambalo Bayern wameona kama fursa kwa upande wao.Mtu anayetajwa kulipambania sana dili hili ni Mtendaji mkuu wa klabu ya Bayern Munich anayefahamika kama Maxi Eberl, Kwani mtendaji huyo ndio mtu aliyemsajili mchezaji huyo ndani ya klabu ya Rb Leipzig mwanzoni mwa msimu uliomalizika.
Kiungo huyo wa kidachi mwenye umri wa miaka (21) amefanikiwa kufanya vizuri ndani ya klabu ya Rb Leipzig kuanzia ligi kuu ya Ujerumani, Lakini pia ligi ya mabingwa barani ulaya jambo ambalo limewavutia miamba ya soka nchini Ujerumani klabu ya Bayern Munich.Inaelezwa kwenye mbio za kumuhitaji Xavi Simons Bayern Munich hawatakua wenyewe kwani klabu ya Rb Leipzig nao wanapambana kuhakikisha kama PSG watamruhusu kiungo huyo kuendelea kutumika kwa mkopo basi wao Leipzig waendelee kummiliki.