Aston Villa imethibitisha kufikia makubaliano na Norwich City ya kumsajili kiungo wa klabu hiyo, Emiliano Buendia. 

Buendia alikuwa mchezaji mwenye mchango mkubwa kwenye kikosi cha Norwich ambapo aliisaidia timu hiyo kuibuka vinara wa Championship na sasa watarejea kwenye EPL msimu ujao. Kiwango thabiti alichokionesha Buendia, kilimfanya kuwa mchezaji bora wa msimu kwenye timu hiyo.

Villa, Villa Yamnasa Emiliano Buendia, Arsenal Wanahaha!, Meridianbet
Emiliano Buendia akiwa na taji la Championship.

Sambamba na Villa, Arsenal ilikuwa kwenye mchakato wa kuiwania saini ya Buendia lakini walizidiwa kete baada ya miamba ya Villa Park kuwasilisha dau la pauni milioni 33 linaloweza kuongezeka mpaka kufikia pauni milioni 40 kukubaliwa na Norwich City.

Kwa sasa, Buendia yupo kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Argentina wakati huu wanapojiandaa na mchezo dhidi ya Colombia. Imeripotiwa kuwa, Buendia atafanyiwa vipimo vya afya muda mfupi baada ya kumaliza mchezo huo kama sehemu ya kukamilisha mchakato wake wa usajili.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa