Naam! Sio bahati, sio ngekewa. Ni mipango ya timu. Aston Villa yafanikiwa kumsajili Diego Carlos.

Carlos anaondoka kwenye timu ambayo inakwenda kucheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa (UEFA) msimu ujao na pia, ni timu ambayo imekua ikishiriki mashindano ya Ulaya kila mara. Villa wana nini?

Ni kama Steven Gerrard anaendelea alipoishia kwenye sajili mbili za nyuma. Kuelekea Julai 1, 2022. Stevie G ameshamsajili Coutinho kwa mkataba wa moja kwa moja akitokea Barcelona, amemsajili Boubacar Kamara akitokea Marseille na sasa, Diego Carlos akitokea Sevilla.

Villa, Villa Yamsajili Diego Carlos., Meridianbet

Wachezaji wote hawa wanatoka kwenye vilabu ambavyo vinacheza mashindani ya Ulaya msimu ujao. Kinachowavutia zaidi Villa Park ni nini? Mipango ya timu? Maslahi? Nguvu ya ushawishi ya kocha? au ni kipi hasa? Haya ni maswali ambayo hayana majibu sahihi lakini, Gerrard yupo kazini, anaandaa kikosi chenye ubora mkubwa kuelekea msimu ujao.

Carlos aliwindwa sana na Newcastle United, Spurs, Chelsea na hata Man United majira ya joto msimu ulioisha na hakuna timu yeyote kati ya hizi ilifanikiwa kumtoa Sevilla. Sasa ni rasmi, anatua EPL msimu ujao akiwa ni mchezaji halali wa Steven Gerrard.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa