Kuna uwepo wa taarifa kwamba nyota wa Chelsea, OLivier Giroud yupo tayari kuwasilisha ombi la kutaka kuuzwa na kuondoka Chelsea.
Wakala wa Olivier, Michael Manuello alipohojiwa alisema; “Kama tukiliangalia mara baada ya msimu uliopita kuisha basi sitokubaliana na wewe sababu, Chelsea ilicheza mwezi juni na julai. Katika miezi sita ya mwisho, Olivier alicheza zaidi ya mechi 16. Na ukiangalia aliyoyafanya kwenye hicho kipindi chote, ameweka rekodi ambayo hautosikia ikiongelewa.”
“Kwasababu kwa umri wa miaka 33 ni nadra sana kuona amefanya yale ambayo aliyoyafanya kwa miezi sita ya mwisho ndani ya Chelsea kwa msimu uliopita. Lakini toka mwezi septemba mambo yamebadilika, ila kuna kitu hakijabadilika kutoka kwa Olivier, uwezo wake haswa akiwa na timu ya taifa ya Ufaransa, akiyapindua yale yanayosemwa dhidi yake.”

“Lakini ukiangalia kitakwimu kabla ya Chelsea kufanya sajili walizozifanya, msimu uliopita walivuna alama 18 kwenye michezo 9. Hizi alama 18 zilikusanywa wakati Olivier akiwa ameanza kwenye michezo 7, uku Chelsea wakifunga magoli 18. Lakini baada ya usajili, toka msimu umeanza, Chelsea imeceza michezo 8 (ligi kuu Uingereza) uku ikifunga magoli 22 na kukusanya alama 15, yani inahitaji ishinde mchezo mwengine wa 9 ili ifikie alama ambazo Olivier Giroud alizifikia msimu uliopita.”
“Katika miaka mitano iliyopita, ukiangalia kuna timu zimeweza kuvuna alama nyingi ndani ya michezo ambayo Chelsea imecheza mpaka sasa uku zikiwa hazijatumia pesa ambayo imetumiwa na Chelsea. Kwa jinsi ambavyo ilimaliza msimu, ulitegemea msimu mpya ukianza watazidi kuwa bora lakini hakuna kitu kikubwa kilichoongezeka.”
“Uwepo wa Kai Havertz, Timo Werner na Hakim Ziyech hakuna kikubwa kilicholetwa licha ya kugharimu pesa nyingi. Lakini pia inashangaza kuona kwa makubwa ambayo Olivier aliyafanya msimu uliopita lakini eti Frank Lampard anamweka Tammy Abraham chaguo la kwanza mbele ya Olivier. Lakini ana haki hiyo kwasababu ni maamuzi yake kama kocha.”
“Lakini naona kabisa kama mambo yakiendelea kama yanavyoendelea kwasasa nafikiri ikifika mwezi desemba tutakuwa kama tulipokuwa kule tulipokuwa mwezi desemba mwaka 2019”
Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.



Povel
Giroud haend tu popote apate nafasi ya kucheza kwn darajan hapati nafasi ya kucheza amekuwah chaguo la 3 chini ya super lampard hvy Kuna mfanya wakala wake hamtafutieh timu ya kucheza mara kwa mara ilikulinda kiwango chake giroud co for me kusepa itakuwah amefany uwamuzi sahihi
Adelta
Mashabiki tunashuru kwa taarifa
Caroline
Giroud mbona ni mchezaji mzuri
Sauda
Giroud anajitahidi kwa kweli.
zeiyana
Ni kweli giround hajapata mda wa kecheza ila kama watampa nafasi nzuri pale kikosi naimani uwezo wake bado hupo hajashuka viwango vyake
Fatina mfingi
Mnamuondoa kwa nn muachen mbon Ni mchezaj mzur ila mpe muda. Na nafac zaid
magdalena
giround abaki tu apo apo chelsea maana sizani kama kuna club itampokea maana hana kiwango kizuri katika uchezaji wake
Hopemwaikuka
Kama unataka kuondoka sawa Ila na umri pia unaanza kukutupa
Lydia Emmanuel Magoti
Vizuri uwamuzi wake ndio umemtuma Kama anataka kuondoka aende kukaa Napo semu moja panakuwa Pana kuzoea Sana anataka kubadilisha upepo akakipige kwingine
Angelina
Nice update
Rahma
Asante kwa tahalifa
Sadick
Giroud ni bora kuliko Abraham, nadhani kocha anamupa nafasi ili kumupa uzoefu zaidi kwa manufaa ya timu hapo baadaye
Nasra
Akafanye vzuri huko aendako
aisha
apate club nzuri ili kipaji chake kisipotee
Fatuma kasomo
Asante kwa taarifa meridianbet
Mwajumah
Anajitaidi sana Giround kwa kweli
Saupha mohamed
Taarifa njema
felister
kila la kheri
Ester jackson
Nafikiri yanaweza kuongea hivyo siwezi kumlaumu ila ninaweza sema kuwa kocha yuko sahihi kufanya hivyo mana wote wanauwezo mzuri hivyo kila mchezaji anamchezesha kwa kiwango sawa kunaambao kwenye timu zao hawajachezeshwa mwaka sasa wapo bench ila yeye bado anapewa nafasi ingawa sio Mara kwa Mara lakini bado anaumuhimu kwenye timu ila uwamuzi ni wao zaidi
Elika
Mbona anahangaika sana huyo giroud
Sania
Makala bomba
Janeflora malisa
Hbr njm
Tatu
Kila la kheri
Mariam mtandama
Habari njema
warda
Amepata penye Riziki