Walinzi Bora Ulaya

Soka ni mchezo unaobadilika siku zote, tangu zama ambazo timu zilikuwa zinacheza kujilinda sana zaidi ya kushambulia hadi pale ambapo wapo kwa sasa. Kwa kiwango kikubwa walinzi ni sehemu muhimu sana katika timu lakini wengi wao wamekuwa hawapati nafasi ya kupata tuzo kubwa duniani pamoja na mchango wao.

Watu kama Carles Puyol, Fabio Cannavaro wanaangaliwa sana kutokana na aina ya mafanikio ambayo walifikia na vikosi vyao ambavyo wamejenga mafanikio makubwa sana na ya heshima sana ila pamoja na hilo wapo walinzi wengine ambao wana mafanikio makubwa sana ndani ya vikosi walivyopitia na wengine wakiwa bado ndani ya vikosi hivyo.

Sergio Ramos (Real Madrid), mchezaji huyo hajaweza tu kushinda tuzo za nje ya klabu hiyo lakini ni kati ya walinzi bora kuwahi kutokea katika historia ya soka. Umakini wake na ubora wake ni kati ya vitu ambavyo havijawahi kushuka kabisa mbele yake. Kila aina ya mshambuliaji hupata shida sana kupata mbinu ya kumpita mlinzi huyo. Kwa utamaduni wake yupo tayari hata kupokea adhabu ya kutolewa nje ya uwanja ili kuzuia kupitwa pale inapowezekana. Kwa hakika ni mlinzi wa aina yake ndani ya klabu hiyo.

Raphael Varane (Real Madrid), raia huyo wa Ufaransa aliyepata mafanikio makubwa sana katika ngazi ya klabu na taifa lake amekuwa sehemu ya mafanikio huko kote alikopita. Ubora wake ni kitu ambacho hakishuki kabisa na uimara wake umeifanya safu ya ulinzi ya Madrid kutawala kwa kipindi kirefu sana barani Ulaya. Mbali na makombe aliyoyanyanyua anakaa katika historia ya pekee sana duniani.

Diego Godin (Atletico Madrid), kati ya vitu vinavyoitambulisha klabu hiyo ni suala lake zima la kuwa na safu bora zaidi kuwahi kutokea ambayo sio rahisi kupenya na mpira na kuwafunga. Ukweli ni kwamba huweza kuruhusu magoli machache sana ndani ya msimu mzima kutofautisha na klabu nyingine ndani ya ligi yao ila uwepo wa Godin ndani ya safu hiyo na ukongwe wake ni vitu ambavyo vina upekee wa aina yake.

Leonardo Bonucci (Juventus), safu imara sana ya ulinzi ndani ya kikosi hicho. Safari yake ya kwenda AC Milan haikuwa na faida sana lakini aliporejea Juventus alirejesha makali yake na kuendelea kuonekana ni mlinzi bora kabisa kwenye soka na kupata heshima duniani kote.

Virgil Van Dijk (Liverpool), kati ya walinzi waliorejesha heshima ndani ya kikosi cha Klopp. Ameweza kuwa na mafanikio ya haraka hadi kuwaaminisha watu ndani ya misimu miwili pekee. Ni aina ya walinzi ambao wana uwezo wa pekee sana na kwa kila analofanya linaweza kuacha alama ndani ya Liverpool.

3 Komentara

    Habar njema

    Jibu

    Nc

    Jibu

    Wako vizuri.

    Jibu

Acha ujumbe