Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amelitaka shirikisho la soka barani Ulaya ‘Uefa’ kuhamishia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenda Uingereza ili kutoa nafasi ya mashabiki kwenda kuishuhudia uwanjani.
Mchezo huo umepangwa kufanyika kwenye nchi ya Uturuki ambayo imewekwa kwenye mstari mwekundu na Uingereza kama nchi yenye maambukizi ya virusi vya corona, hivyo mashabiki wa Chelsea na Manchester City watakaokwenda kushuhudia fainali hiyo watalamizika kuingia gharama nyingine za kujitenga hotelini kwa siku 10 watakaporejea kutoka Istanbul baada ya fainali hiyo ya Mei 29.
Waziri Mkuu Johnson aliambia SunSport: “Ligi ya Mabingwa Ulaya ni michuano mikubwa kabisa ya ngazi ya klabu kwenye soka la Ulaya. Na timu mbili za England zitacheza fainali, hivyo itakuwa aibu kubwa kama mashabiki watashindwa kwenda kuhudhuria.
“Itakuwa jambo zuri sana kama fainali itafanyika hapa. Nataka kuwasaidia mashabiki wa timu hizo zote mbili kupata fursa ya kwenda uwanjani kutazama fainali.”
Kiongozi huyo wa serikali ya Uingereza alisema mechi hiyo ikipigwa England, kutakuwa na uhakika wa mashabiki wapatao 15,000 kuhudhuria.
TENGENEZA FAIDA KUPITIA MCHEZO WA TITAN DICE UKIWA NA MERIDIANBET KASINO
Unapokuwa kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, huna sababu ya kucheza kwa mashaka. Titan Dice, ni mchezo unaweza kukupatia mamilioni kwa mzunguko mmoja!
Amesema jambo jema ila sasa vipi kuhusu covid 19 imeisha au
Dah sio poa
Coronavirus sio poa
Duuh sio poa