Yanga: Tutaingia na Nguvu Nyingi

KUELEKEA mchezo wa Dabi ya kariakoo dhidi ya Simba, Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amefunguka kuwa wataingia na nguvu nyingi kwenye mchezo huo.

Mchezo huo unatarajiwa kupigwa Oktoba 23 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar saa 11:00 jioni.

Akizungumzia maandalizi yao, Kaze alisema “Tumerejea mazoezini baada ya kupoteza mchezo wa michuano ya Klabu bingwa dhidi ya Al Hilal.

“Tulianza kuwajenga wachezaji kisaikolojia kutokana na kupoteza mchezo uliopita kwani haikuwa rahisi kwa upande wetu.

“Inabidi tuingie kwenye mchezo huo kwa nguvu nyingi kwa ajili ya kuhakikisha tunapata matokeo kwani tunajua mashabiki wetu wanahitaji kufurahi.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.