Kufungwa kwa dirisha la usajili mara zote sio ishara kwamba kila kitu kinapoa na fununu zinaishia kwa wakati huo. Hiyo huwa ni ishara ya kujiandaa kwa sajili nyingine zinazokuja mara baada ya kukosa lile hitaji la klabu kwa wakati huo. Jambo linaloendana na hilo ni kuwepo kwa majina ambayo bado yanafukuziwa. Zifuatazo ni fununu za soka barani Ulaya:
Che Adams
Uwepo wa Cenk Tosun na Dominic Calvert-Lewin kwa wakati ambao washambuliaji wawili Richarlison na Gylfi Sigurdsson kuwa nje ya uwanja yanaonekana yanawapa shida sana wakongwe wa soka nchini Uingereza kushindwa kutambua na kupata nafasi ya kucheka na nyavu kwa idadi kubwa ya magoli hivyo wapo sokoni kufukuzia jina la Adams ambaye anakipiga pale Birmingham City wakiamini kama mchezaji halali kuziba nafasi.
Luciano Acosta
Jicho la Manchester United kwa sasa lipo wazi kule MLS kuangalia kama mchezaji huyo anaweza akaendana na falsafa za kikosi chao kutokana na uwezo wao mkubwa. Kwa sasa nyota huyo anakipiga na klabu ya DC United na makali yake yanaonesha ana kitu cha pekee na uwezo mkubwa kufanya makubwa sana.
Maxi Gomez
Nyota huyo kwa sasa anakuja juu. Sio West Ham pekee waliiona nafasi yake klabuni hapo lakini pia yeye mwenyewe anajiona thamani yake imepanda baada ya kuanza kuhusishwa na miamba wawili wa soka wanaoonekana kumnyemelea na kuhitaji kuona zaidi uwezo wake ndani ya klabu zao kama Real Madrid na mahasimu wao wa soka, Barcelona. Kama hilo halitoshi nyota huyo bado ana nafasi ya kufanya makubwa zaidi ili kujenga uaminifu wake.
Edin Dzeko
West Ham bado wanaonekana kuwa mbioni kutanua kikosi chao kwa kumuweka kwenye matamanio mshambuliaji wa Roma ili aweze kutua kikosini hapo. Nyota huyo amekuwa na msimu rafiki sana ndani ya kikosi chake tangu ajiunge na miamba hao wa soka. Mancini anaonekana kufurahia sana nafasi ya mchezaji huyo na furaha yake itakamilika kama angefanikishiwa mipango yake.
Hizo ni baadhi ya taarifa zinazoendelea kugonga vyombo vya habari zaidi kutokana na klabu kuona kuna uhitaji mkubwa wa wao kupata wachezaji watakaosaidia vikosi vyao kusonga mbele na angalau kuibuka na makombe zaidi ya kuishia kushiriki kwenye michuano wanayokuwa wamefuzu kuwemo. Hiyo ni njia pekee ya klabu kujimudu kupitia soka.


Povel
Habar njema