EPL: Hakimu Dhaifu wa Ubingwa

Siku pekee ambayo mashabiki wa soka watatumia nguvu zao na maombi yao yote kumuombea Manchester United aweze kushinda mechi yake atakayokutana na Manchester City ni leo hii. Nguvu ya ushindi wa mechi hiyo ni kigezo pekee cha Liverpool kukwea juu na kunyanyua kombe hilo.

Manchester United atakuwa na mashabiki wengi sana kuwahi kutokea katika mechi yake hiyo pamoja na mapungufu yake ya siku za usoni na ni jambo la pekee pia kwao kama wataweza kuondoa wasiwasi uliowafunika mashabiki zake juu ya mwenendo wake wa kupata ushindi kwenye mechi nyingi anazoingia uwanjani.

United wanarudi uwanjani wakikumbuka kichapo walichokipokea mbele ya Everton wikiendi kitu ambacho kwa hakika ni jambo ambalo limewahuzunisha mashabiki wengi na kuona kabisa matumaini ya kusogea kwenye nafasi nne za juu yanaendelea kuyeyuka taratibu kutokana na kichapo hicho.

City wapo kwenye fomu nzuri zaidi wakiutetea ubingwa.
City wapo kwenye fomu nzuri zaidi wakiutetea ubingwa

Ugumu na uzuri wa mechi hiyo ni kutokana na uhitaji wa alama kwa kila klabu inayoingia uwanjani kupigana. City anaingia akiwa na tamaa kubwa ya kutaka alama tatu muhimu pia akiwa tayari na morali ya juu baada ya kushinda mechi yake dhidi ya Spurs hivyo kwake mechi hiyo ni zaidi ya fainali kuelekea ubingwa.

Lakini upande wa United pia wanaiangalia mechi hiyo kwa jicho la pekee na aina yake kutokana na kuhitaji alama tatu muhimu ili kuweza kuendelea kuleta upinzani mkubwa kutafuta nafasi ya kushiriki klabu bingwa. Pia, nyuma yake akiwa amebeba sala nzima za mashabiki wa Liverpool ambao wanamtegemea kwa kiwango kikubwa.

Miongoni mwa wachezaji wa klabu ya Liverpool wameweka hisia zao wazi kwamba kuelekeamechi hiyo kwa hakika watakuwa upande wa Manchester United kwa sababu wanatamani sana kwa nafasi yao City apoteze ili wao waweze kuibuka mabingwa kwenye kombe hilo la ligi.

Baadhi ya nyota hao ni Trent Alexander-Arnold ambaye anasema kwa nguvu zake zote atawapa nguvu zake za kushangilia United kwa sababu anajua ushindi wao kwenye mechi hiyo ni kigezo pekee cha wao kuibuka mabingwa mwaka huu; kinyume na hapo watawafanya City waweze kukaa juu na kuchukua ubingwa huo.

Ameweza kuwataja watu kama Rashford kwa kusema kwamba anategemea wataweza kufanya jambo ambalo kwa hakika litawasaidia wao kushinda mechi na baadaye watakuwa wametengeneza kitu cha faida sana kati ya pande hizo mbili. Kwake wakati huu anahitaji nguvu ya United lakini haimaanishi kwamba ni shabiki wa kudumu wa klabu hiyo.

Makala iliyopita

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.