Kylian Mbappe Shakani Kuwakosa Real Madrid

Mshambuliaji nyota wa timu ya Paris St Germain Kylian Mbappe amepata majeraha ya mguu akiwa mazoezini na bado kuna wasiwasi ikiwa atakuwa sawa kuwavaa klabu ya Real Madrid kwenye mzunguko wa pili wa hatua ya kumi na sita bora siku ya Jumatano kwenye ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Mbappe ndio mfungaji pekee wa goli la Paris St Germain kwenye mchezo wa kwanzaa na kufanya mchezo kuisha kwa 1-0 mwezi February.

Kylian Mbappe
Kylian Mbappe

“Kylian Mbappe anasumbuliwa na mshtuko wa mguu wa kushoto alioupata kwenye mazoezi hii leo,” waraka uliotolewa na PSG siku ya jumatatu.

“Alitibiwa mchana wa leo, wataalamu wanajihakikishia na watamfanyia tena vipimo baada ya saa 24.”

Mbappe ameukosa mchezo wa siku ya Jumamosi ambapo psg walipoteza dhidi ya Nice kwa 1-0 kwenye ligi kuu ya ufaransa Ligue 1 kutokana na adhabu, ambapo PSG waliweza kupiga mashuti mawili tu ndio yaliolenga golini.

PSG walikataa offa mbalimbali kutoka kwa Real Madrid kwa ajiri ya kuweza kumbaiksha mbappe mwenye miaka 23, ambaye mwisho wa msimu huu anaweza kuondoka kama mchezaji huru baada ya mkataba wake kuisha.


VUNA MKWANJA NA SHINDANO LA EVOPLAY SPRING AWEKING

Mchongo mpya mjini ni Shindano la Evoplay Spring Aweking katika kasino maridhawa za meridianbettz. Pata mgao wako wa TSh 25,000,000  katika michezo kibao ya kasino na sloti ziliyochaguliwa kushiriki.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

Acha ujumbe