Julio Aanzisha Zoezi la kuchangisha 

Kocha Msaidizi wa Namungo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza kwa ajili ya kumchangia aliyekuwa mchezaji wa Polisi Tanzania Gerald Mdamu kufanyiwa matibabu.

Mdamu alivunjika miguu yote miwili kwenye ajali ya basi la Polisi Tanzania wakati likitoka mazoezini kuelekea kambini.

Akizungumzia hilo, Julio amesema kuwa: “Mimi ndiye nilimsaidia Mdamu kufika hapa alipo sasa sitamani kuona anashindwa kucheza mpira baadae.

“Ningewaomba wadau mbalimbali wa soka waweze kumchangia Mdamu aende Italia kwa ajili ya kupatiwa matibabu ili aweze kurejea uwanjani tena.”

Gerald Mdamu hii sio mara ya kwanza kuchangiwa tokea apate ajaari hiyo, awali timu ya Polisi Tanzania kuna taarifa zilikuwa zikisambaa kuwa imemtelekeza mchezaji huyo kwa kushindwa kulipia matibabu yake, ambapo ilipelekea achelewe kurudi uwanjani mpaka sasa.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.