Everton Yathibitisha Kukamilisha Usajiri wa Idrissa Gueye

Klabu ya Everton imethibitisha kukamilisha usajiri wa kiungo wa kimataifa kutoka senegal Idrissa Gueye ambaye alikuwa anaichezea klabu ya Paris Saint Germain ya ufaransa na anatarajiwa kusaini kandarasi ya miaka miwili.

Idrissa Gueye awali alijiunga na everton akitokea klabu ya Aston Villa mwaka 2016 ambapo aliichezea klabu hiyo michezo 108 ba kufunga magoli manne tu kabla ya kujiunga na klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa mwaka 2019.

Paris Saint Germain walilipa kiasi kinachokadiriwa kufikia £30million ili kuweze kuhakikisha Idrissa Gueye anajiunga kwenye dimba la Parc des Princes mwaka 2019. Gueye amefanikiwa kushinda makombe mawili ya ligi kuu ya Ufaransa kabla ya kurejea tena Uingereza msimu huu.

Gueye akifanya mahojiano kama mchezaji wa Everton alisema kuwa anaipenda klabu na ndiyo timu pekee ambayo alitaka kujiunga nayo baada ya kuachana na klabu ya Paris Saint Germain.

Hakuna jambo bora kama kurudi nyumbani, Nina furaha kuwa hapa Everton tena, kusaidi na kufanyakazi kwa juhudi. Nitatoa roho yangu kwa ajiri ya hii timu.” Gueye alisema.

“Kurudi hapa ilikuwa ni muhimu kwangu kwa sababu najihisi niko nyumbani. Nimekuwa mikiifwatilia hii timu kila wiki na kuingalia jinsi inavyocheza. Kwangu, hakuna sehemu bora kuliko Everton. Ndiyo maana nimechagua kurudi hapa.”

Taarifa ya awali kuhusu ada ya usajiri wa Gueye ilikuwa na thamani inayokadiriwa kufikia £8milion, lakini maelezo kutoka Skysport inaeleza kuwa ada ya mchezaji huyo ni £2milion.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.