Bamba Dieng mshambuliaji wa kimataifa wa Senegali na klabu ya Olympique Marseille inayoshriki ligi kuu ya Ufaransa amefeli vipimo vya afya katika klabu ya Nice pia ya nchini Ufaransa.
Nyota huyo wa kisenegali alikua anahitajika na klabu ya Leeds United ambao walionekana kua karibu zaidi kumpata mshambuliaji huyo na mshambuliaji huyo alifikia hatua ya kwenda uwanja wa ndege akijianda kuelekea klabu ya Leeds lakini aliamua kupiga chini ofa hiyo na kuamua kuelekea klabu ya Nice.
Wakati Bamba Dieng ameamua kupiga chini ofa ya Leeds na kuamuan kuelekea Nice ndipo changamoto ilipotokea kwa msenegali huyo pale ambapo alifeli vipimo vya afya katika klabu ya Nice.
Hali hii imemfanya mchezaji huyo raia Senegal kubakia katika klabu yake ya Olympique Marseille.

