Arsenal wakiwa wageni katika dimba la Old Trafford jioni ya leo wanakwenda kutafuta ushindi wao wa saba kwenye dimba hilo kwa miaka 40.
Klabu hiyo yenye maskani yake jijini London imeshinda michezo sita pekee kwenye ligi kuu ya Uingereza katika dimba la Old Trafford ambapo michezo mingine iliobakia wakifungwa na kuambulia sare hivo leo hii wakiwa kwenye kiwango bora kabisa wanakwenda machinjioni kutafuta ushindi wao wa saba ndani ya miaka 40.
Vilabu hivi kwenye rekodi za jumla wamekutana mara sitini huku United wakifanikiwa kushinda mara 25 huku Arsenal wakishinda mara 17 michezo nane iliosalia ikiisha kwa sare.
Klabu ya Arsenal wanakwenda kwenye mchezo huu wakiwa wameshinda michezo yao yote mitano ya awali kwenye ligi kuu ya Uingereza huku wakiwa kileleni huku wenyeji wao Man United wakiwa wameshinda michezo mitatu mfululizo baada ya kupoteza michezo miwili ya awali hivo unatarajiwa kua mchezo mgumu sana kwani hawa ni mahasimu wa muda mrefu.
Washika mitutu wa London wakifanikiwa kushinda leo katika dimba la Old Trafford wanaongeza idadi ya ushindi kwenye dimba hilo ambalo limeonekana kua chungu kwao wakipata ushindi mara sita tu kwa miaka 40.

