Gary Neville Amsifu Conte.

Gary Neville gwiji wa zamani klabu ya Manchester United amesifu uwezo wa kocha wa sasa klabu ya Tottenham hotspurs.

Gwiji huyo ameonesha kuvutiwa na kiwango kinachooneshwa na klabu hiyo yenye maskani yake jijini London ambayo anaamini uwezo ubora huo umechangiwa na ubora wa mwalimu huyo raia wa Italia, Hii inawezekana na uzoefu wa mwalimu huyo ndani ya ligi kuu ya Uingereza ambapo ameshafundisha klabu  ya Chelsea pia ya jijini London ambapo pia amewahi kubeba ubingwa na Chelsea mwaka 2017.

gary nevilleNeville anaamini pia Conte kaleta hamasa na hali yaupmbanaji ndani ya klabu hiyo na kuongeza Conte amepata hamasa hizi kutoka kwa makocha kama Rafa Benitez na Jose Mourinho.

Ikumbukwe miezi kadhaa nyuma Neville  alipinga uamuzi wa klabu yake ya zamani ya kutaka kumuajiri kocha huyo wakati mwalimu wa United wakati huo Ole Gunnar Solskjaer anafanya vibaya na hata pale alipofukuzwa kazi.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.