Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United Gary Neville anaona kocha wa Paris Saint Germain kuwa ni chaguo sahihi kuweza kuinoa klabu hiyo dhidi ya kocha wa klabu ya Ajax Erik ten Hag.
Mauricio Pochettino ameshawai kuhusishwa kuhitajika kuionoa klabu ya Man Utd mara mbili, mara ya kwanza ni mwaka 2016 ambapo Jose Mourinho ndie aliepewa majukumu ya kuinoa klabu hiyo, huku mara ya pili mwaka 2018 Ole Gunnar Solskjaer alikifanikiwa kuchukua mikoba dhidi yake.
Gary Neville alianzisha mjadara kwenye mtandao wa Twitter, ambapo aliwataka mashabikiwa wa klabu ya Man Utd kupiga kula kuhusu nani wangependa kuwa kocha ajaye kwenye klabu hiyo leo siku ya jumatano.
Gary Neville, yeye mwenyewe kwenye ukarasa wake wa Twitter, aliweka wazi kuwa angependa kuona Pochettino ndiye anakuwa kocha wa timu hiyo licha ya mashabiki wengi wa klabu hiyo kutaka Erik ten Hag kuinoa timu hiyo.
“Nitakwenda na Pochettino lakini mashabiki wengi wa United wanampenda Erik ten Hag kuchukua mikoba ya kuinoa timu hiyo. Ni chaguo la wazi kati ya wawili hao.” Alisema Neville.
Hivi karibuni klabu ya Man Utd walimfanyia mahojiano Erik ten Hag ili kuona ikiwa anaweza kushika mikoba ya kuinoa klabu hiyo.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.