Bingwa mtetezi wa mkanda wa Dunia Oleksandr Usyk ameripotiwa kuwa ataondoka nchini mwake Ukraine kwaajili ya kuanza mazoezi kuelekea pambano la marudiano dhidi ya Anthony Joshua litakalo fanyika majira ya kiangazi.

Usyk Kuondoka Ukraine Kwa Maandalizi ya Marudiano na AJ

Kwa mujibu wa ESPN Usyk ataanza mazoezi nchini Poland kwaajili ya kutetea mkanda wa uzani dhidi ya bondia wa Uingereza Anthony Joshua na promota wa AJ Eddie Hearn alisema kwamba watampa Usyk muda kutosha kwaajili ya kujiandaa na pambano hilo la marudiano.

Usyk alijiunga na jeshi la Ukraine baada ya jeshi la Urusi kuvamia nchi hiyo mwezi Februari, bingwa huyo alisema:

“Kwa kweli sijui ni lini nitarejea kwenye ulingo,” Usyk aliiambia ESPN mapema Machi.

“Nchi yangu na heshima yangu ni muhimu zaidi kwangu kuliko mkanda wa ubingwa.”


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa