Urusi Watangaza Nia ya Kuandaa Euro 2028 au 2032

Urusi wametangaza nia ya kutaka kuanda michuano ya Euro 2028 baada ya Uingereza na washarika wake kuwasilisha maombi ya kuandaa michuano hiyo licha ya nchi hiyo kuwekewa vikwazo.

Timu za taifa la Urusi na vilabu vyake vyote kwa sasa vimezuiliwa na FIFA na UEFA kushiriki mashindano yote yanayoandaliwa na taasisi hizo, kutokana na Uvamizi uliofanywa na nchi hiyo dhidi ya Ukraine.

Urusi japokuwa na vikwazo vyote walivyowekewa, bado haijawazuia kuweza kurudi nyuma kwenye kutaka kushindana ili na wao waweze kupata nafasi ya kuandaa mashindano hayo makubwa barani Ulaya, ambapo mwisho wa kupokea maombi ni siku ya jumatano.

Kwenye chapisho lilotolewa kwenye mtandao wa shirikisho la mpira wa miguu nchini Urusi, lilielezea idadi ya matokeo ya kikao kilichofanyika leo jumatano, ikiwemo, maamuzi ya kutaka kuandaa mashindano ya Euro 2028 au 2032 nchini Urusi.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe