UEFA Kuvunja Mkataba wa Matangazo ya Tv kwa Michezo ya Kimataifa na Urusi

Shirikisho la mpira barani Ulaya UEFA linafanya mchakato wa kuvunja mkataba wa haki ya matangazo ya kuonesha michezo ya kimataifa na nchi ya urusi ndani ya wiki hii hii ikihusisha michezo ya kirafiki ikiwemo Uingereza, Switzerland na Ivory Coast.

Kulingana na taarifa iliyotoka leo, bado kuna mashirika ya nchini Urusi yanahaki ya kuonesha michezo ya kimataifa mpaka sasa, lakini UEFA wanaangali ni kwa jinsi gani wanaweza kuzuia michezo yote isionyeshwe kwenye nchi ya Urusi.

UEFA imeshikilia haki ya matangazo ya wanachama wote 55 kwenye shirikisho hilo, kwa hiyo hata FA haina uwezo wa kupinga michezo yake isionyeshwe au ionyeshwe nchini Urusi.

Timu za taifa za Urusi na klabu zake zote zimezuiliwa kushiriki mashindano yanayoandaliwa na FIFA na UEFA, ikiwemo michezo ya kufuzu kombe la dunia, baada ya rufani yao kukataliwa na mahakama ya usuruhishi ya kimichezo CAS.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe