Juventus walijiamini sana? Juventus waliamini wangeweza kuweka sawa maswala ya kimkataba na nyota wao anayemaliza muda wake, Paulo Dybala.
Kwa mujibu wa gazeti la La Stampa, Juventus walikuwa wameandaa shuguli ya kusherehekea kuongezwa kwa mkataba wa Paulo Dybala kabla ya kubadilisha mkakati na kuamua kumwachilia Staa huyu aondoke.
Ilitangazwa jana kuwa mkutano wa hivi karibuni kati ya wakala wa Dybala na klabu, ambao pia ilikuwa wa mwisho, ulishindwa kuleta mwafaka bora kuhusu mkataba mpya, klabu haikutoa ofa nyingine.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina ataondoka kama mchezaji huru pale mkataba wake utakapokamilika Juni 30.
Ilikuwa ni mabadiliko makubwa kutoka kwa hali hiyo miezi michache tu iliyopita, huku La Stampa ikidai kuwa Juventus walikuwa wameandaa tafrija ya kusherehekea kuongezwa kwa mkataba wa Staa wao Nambari 10.
Mambo yalibadilika kutokana na kupungua kiwango kwa timu kwa ujumla katika miezi ya mwisho ya 2021, na matatizo ya misuli yanayoendelea kwa Dybala na pia uwekezaji wa Dusan Vlahovic kutoka Fiorentina.
Inaripotiwa kuwa majeraha hayo ndiyo yaliyokuwa yakisumbua zaidi, ambapo awali Juve walitoa kandarasi fupi ya miaka mitatu na chaguo la kuongeza, au kupunguza mshahara na bonasi kufuatia jumla ya mechi atakazocheza.
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.