Xavi na Ndoto za Dembele Kubaki Barcelona

Kocha wa klabu ya Barcelona Xavi hernandez bado anaimani kuwa mchezaji wa kimataifa kutoka nchini Ufaransa Ousmane Dembele atasaini mkataba mpya na klabu hiyo baada ya msimu kuisha.

Dembele amekuwa kwenye mzozo na klabu ya Barcelona kuhusu maswala ya kimkataba, huku mara kadhaa amekuwa na akishutumiwa yeye na wakala wake kukwamisha maongezi ya kimkataba.

Xavi
Xavi hernandez

Kulingana na taarifa kutoka Diario AS, Xavi Hernandez bado hajakata tamaa kwa winga huyo wa kifaransa na anatumai kuwa Dembele atakubali offa ya mkataba mpya, baada ya klabu hiyo kufanya marekebisho ya vipengere vya kimkataba, na pia hivi karibuni wamefanya mabadiliko kwa mara ya nne kwenye mkataba huo.

Dembele atakuwa huru baada ya msimu kuisha na anaweza kufanya mazungumzo na klabu yoyote, ambapo vilabu vikubwa tayari vishaanza kuonesha nia ya kuhitaji huduma yake kama PSG, Manchester United, Chelsea na Newcastle United, huku mazungumzo ya kusaini mkataba mpya yakiwa bado wazi kwa klabu ya Barcelona.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe