"Ousmane Dembele Atasalia Barcelona" -Rafa Yuste

Makamu wa rais wa Barcelona Rafa Yuste amesema kuwa Ousmane Dembele bado anaweza kusalia Camp Nou kutokana na maelezo yaliyotolewa na Fabrizio Romano. Pia amehakikishia klabu hiyo inafanya kazi kwa bidii ili kurekebisha kandarasi za Gavi na Ronald Araujo.

Dembele alijiunga na Barcelona akitokea Borussia Dortmund msimu wa joto wa 2017 na mkataba wake na klabu hiyo ya Catalan unatarajiwa kuisha mwishoni mwa msimu huu. Mazungumzo hayafanyiki lakini winga huyo anaonekana kuimarika chini ya Xavi Hernandez.

Wote wawili Gavi na Araujo ni miongoni mwa nyota wachanga wa Barcelona na wako kwenye uwezekano wa nyongeza kubwa ya malipo; wametoka mbali kuwa wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza.

Yuste alithibitisha kwamba Barcelona wako tayari kuanza tena mazungumzo na mawakala wa Dembele na wanafanya bidii kufikia makubaliano na Gavi na Araujo. Muda tu utaonesha ikiwa wanaweza kupata suluhu na vijana hao muhimu.

“Ikiwa Ousmane Dembele ataendelea kuwa vizuri, tunaweza kukutana na mawakala wake na anaweza kubaki. Tunafanya kazi kwa uwezo wetu wote kuwabakiza Gavi na Araujo klabuni hapa. Nina matumaini. Wachezaji wana furaha.” – Rafa Yuste


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe