Tottenham wamekasirishwa na kitendo cha kibaguzi alichofanyiwa mchezaji wao Richarlison wakati yupo katika majukumu ya kulitumikia taifa lake la Brazil.
KLabu ya Tottenham imeonesha kuchukizwa na kitendo akichofanyiwa mchezaji wao huyo raia wa Brazil katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Tunisia baada ya klabu hiyo kulaani kitendo hicho kupitia mitandao yao mbalimbali ya kijamii.
Katika mchezo wa kirafiki uliopigwa katika dimba la Parc de Princes nchini Ufaransa kati ya Brazil na Tunisia uliomalizika kwa Brazil kushinda kwa magoli matano kwa moja mchezaji Richarlison alikumbana na kitendo cha kibaguzi baada ya kurushiwa ndizi akiwa uwanjani katika mchezo huo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil nae ameonesha kuchukizwa na kitendo hicho baada ya kuandika kwenye mtandao wake wa kijamii na kuandika hivi “Itaendelea hivi mpaka visa kama hivi vitakapoadhibiwa”.
Richarlison ambae ameungwa mkono na wachezaji wenzake wa Brazil pamoja na Tottenham huku klabu yake pia ikitoa neno “Tumechukizwa na kitendo cha kinyanyasaji kwa Richarlison kwenye mchezo wa jana usiku kati ya Brazil na Tunisia” Tottenham waliandika hivi kupitia mtandao wao wa Twitter.
“Hii haina nafasi kwenye soka, au popote tunasimama na wewe Richy” Hii sio mara ya kwanza kwa mchezaji wa kibrazil kukumbana na kityendo cha ubaguzi wa rangi,Hali imeshawahi kumkuta mchezaji wa zamani wa Barcelona Dani Alves kutupiwa ndizi uwanjani.

