Uhamisho wa Cristiano Ronaldo kwenda Al Hilal ya Saudi Arabia ulishindikana kutokana na kufungiwa kusajili wachezaji kwa timu hiyo, kulingana na madai ya Rais wa klabu, Fahad ben Nafel.

Sportsmail iliripoti siku ya mwisho ya usajili kuwa timu hiyo yenye maskani yake Riyadh ndiyo pekee iliyowasilisha ofa kwa nyota huyo wa Manchester United, baada ya kutangaza kutaka kuondoka msimu huu wa joto kutokana na timu yake kutokucheza Uefa.
Naye Ben Nafel, ambaye aliidhinisha mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya paundi milioni 2 kwa wiki na paundi milioni 210 kwa jumla, pamoja na ada ya uhamisho ya paundi milioni 25, alisisitiza kuwa nyota huyo wa Ureno alifurahishwa na hatua hiyo ya ‘kanuni’, licha ya ripoti kwamba alihisi. ilikuwa hatua ya chini na hamu yake ya kucheza katika Ligi ya Mabingwa.

Alikiambia kituo cha YouTube cha Thamanya: “Ndiyo, tulijadiliana na Ronaldo. Tatizo halikuwa kwenye pesa au kanuni.”
“Al Hilal ina uwezo wa kuleta nyota wa dunia, lakini ni katika uamuzi wa Kituo cha Usuluhishi cha Michezo ndio ulituzuia kusajili wachezaji. Hatukuacha kufanya mazungumzo na wachezaji licha ya uamuzi wa kupigwa marufuku, lakini tulikuwa tunachelewesha kuingia hatua ya mwisho ya mazungumzo hadi marufuku hiyo ilipoondolewa.”
Ofa hiyo ingemfanya Ronaldo mwenye umri wa miaka 37, ambaye bao lake pekee la klabu msimu huu hadi sasa lilikuja dhidi ya timu ya Moldova, Sheriff Tiraspol kwenye Ligi ya Europa.

Al Hilal walipigwa marufuku ya uhamisho mwezi Mei baada ya kiungo wao Mohamed Kanno, kubadili mawazo yake ya kuhamia Al-Nassr dakika za mwisho, huku kandarasi ikiwa tayari imesainiwa na klabu zote mbili.
Al Hilal, inayonolewa na Ramon Diaz, ina wachezaji kama kiungo mshambuliaji wa zamani wa West Bromwich Albion Matheus Pereira, mshambuliaji wa zamani wa Atletico Madrid Luciano Vietto, mshambuliaji wa Mali Moussa Marega na mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo aliyewahi kupita United.

