Dejan Georgijevic mshambuliaji wa Simba amethibitisha kuachana na klabu hiyo baada ya kuposti kwenye mtandao wake wa kijamii baada ya muda mfupi wa kuwepo klabuni hapo.
Siku kadhaa nyuma kumekua na stori ya kutokua na maelewano na baadhi ya wachezaji ndani ya klabu hiyo na hii imeonekana siku kadhaa baada ya kutokua na maelewano na mchezaji mwenzake wa klabu hiyo raia wa Ghana Augustine Okrah katika mchezo wa kirafiki huko Visiwani Zanzibar.
Kumekua na baadhi ya taarifa kua mchezaji huyo amekua akilalamikia uongozi kua wachezaji wenzake wanamnyima pasi uwanjani kitu ambacho ameshindwa kukivumilia kutokana na tabia hiyo ya baadhi ya wachezaji wenzake.
Dejan Georgijevic ameeleza sababu ya kuvunja mkataba na klabu hiyo ni kutokana na timu hiyo kutokutimiza makubaliano ya kimkataba waliyoingia baina yao hivo kuamua kusitisha mkataba huo.
Dejan Georgijevic mshambuliaji huyo aliepata umaarufu sana siku za karibuni baada ya kutambulishwa katika siku ya Simba Day na “Neno la Mlete Mzungu” likawa maarufu sana baada ya pale na kumfanya mshambuliaji huyo kupata umaarufu,kutambulika na kupendwa na Watanzania kabla ya leo kutangaza kuachana na timu hiyo.

