Eric Ten Haag United Inahitaji Muda ili Ifanye Vizuri.

Kocha wa Manchester United Eric Ten Haag amesema itachukua miezi kadhaa ili klabu hiyo iweze kurudi kwenye ubora na kuwasha moto tena kama ilivyokua miaka kadhaa iliyopita.

eric ten haagMashabiki wa Manchester United walianza kupata matumaini baada ya klabu kupata ushindi katika michezo minne ya ligi kuu Uingereza kabla ya kupewa kipigo cha aibu wikiendi iliyoisha dhidi ya mahasimu zao klabu ya Manchester City kitu kilichokuja kuchafua hali ya hewa tena klabuni hapo.

Vijana hao wa Eric Ten Haag jana walipata ushindi katika michuano ya Uefa Europa League kwa jumla ya mabao matatu kwa bila dhidi ya klabu ya Ommo Nicosia kutoka Cyprus huku wakikabiuliwa na mchezo mgumu dhidi ya klabu ya Everon katika ligi kuu ya Uingereza siku ya jumapili.

Kocha huyo wa zamani wa Ajax ameeleza timu yake itachukua muda ila kufikia kiwango anachokitarajia “Tumeiona timu dhidi ya Liverpool,Arsenal lakini ianatupasa kufanya tulichofanya kwa msingi thabiti,hilo ndo tunapaswa kulifanyia kazi kwasa”.

eriic ten haag“Pia haitachukua siku, Itachukua wiki au miezi ili kuweza kusimamisha timu” Alifunguka Eric akielezea namna ambavyo timu hiyo inahitaji muda ili kufanya vizuri kwani yeye anaona sio jambo la haraka kuirudisha timu kwenye mstari.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.