Lionel Messi Kuikosa Reims Wikiendi Hii.

Nyota wa klabu ya PSG Lionel MessiΒ  mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Ufaransa ataukosa mchezo wa kesho jumamosi dhidi ya klabu ya Reims kutokana na majeraha.

lionel messiLionel Messi ataukosa mchezo huo baada ya kupata majeraha ya mguu wake na kocha wa klabu hiyo Christopher Galtier amethibisha hilo.

Mshambuliaji huyo ambaye alifunga bao zuri katikati ya wiki wakati klabu yake ikipata suluhu ugenini dhidi ya Benfica na kua mchezaji wa kwanza kufunga timu 40 tofauti kwenye michuano ya mabingwa ulaya.

“Kutakua na mabadiliko, Messi hatokuepo dhidi ya Reims lakini ataanza mazoezi jumapili asubuhi” Alieleza Galtier wakati anafanya mahojiano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo.lionel messiKutokana na kauli ya kocha Galtier inaonesha Lionel Messi hajapata majeraha makubwa na atarejea uwanjani mapema sana kuendelea kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake jijini Paris.

Acha ujumbe