Taarifa zinasema kuwa nyota wa zamani wa Barcelona, Lionel Messi ataelekea MLS msimu wa joto wa 2023.

Hii ni kwa mujibu wa mwanahabari Alex Candal alipokuwa akizungumza na Direct TV kupitia Diario AS siku chache zilizopita. Taarifa inasema kuwa Messi atatumia msimu mmoja zaidi na Paris Saint-Germain kabla ya kuondoka.

Staa huyu anatajwa kuwa na mpango wa kununua hisa 35% ya Inter Miami franchise, inayomilikiwa na David Beckham, mara tu mkataba wake na PSG utakapomalizika.

Messi anataka kutumia msimu mmoja zaidi barani Ulaya, ili kuhakikisha yuko katika fomu nzuri kuiongoza Argentina kwenye Kombe la Dunia huko Qatar mwaka huu.

Kwa sababu hiyo bila shaka ni dhamira yake kuu. Messi aliiongoza Argentina kutwaa ubingwa wa Copa America msimu uliopita wa kiangazi, dhidi ya Brazil kwenye fainali iliyofanyika Rio de Janeiro na kuipa Argentina taji la kwanza tangu 1993.

Argentina watakuwa miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa ya kushinda tuzo kubwa kuliko zote kule Qatar na Messi atahitaji kuwa kwenye kiwango bora ni jambo muhimu.

Lionel Messi

Lionel Messi alijiunga na PSG kutoka Barcelona msimu uliopita wa joto baada ya klabu hiyo ya Catalan kushindwa kumudu gharama za kuongeza mkataba wake. Amecheza vizuri msimu huu lakini si kwa kiwango chake alichotarajiwa.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa