Rais wa Barcelona Joan Laporta amezungumza kuhusu nafasi ya Neymar Junior kuondoka Paris Saint-Germain na kurejea Camp Nou katika maoni yake kupitia L’Esportiu. Alichosema hakitaenda vyema kwenye Parc des Princes akitaja kuwa Neymara anakuwa kama mtumwa PSG.
“Nani hampendi Neymar? Ni mchezaji wa kipekee, Lakini wachezaji hawa wote kurejea Barcelona siku moja inafaa kuwa bure. Wachezaji ambao wamesajiliwa kwa vilabu kama PSG karibu wameamua kusaini kwa ajili ya utumwa wao. Kwa ajili ya pesa.” -Joan Laporta
Neymar anaripotiwa kuwa ziada kwenye mahitaji ya kikosi pale Parc des Princes kabla ya majira ya joto ya msimu mpya.

Kylian Mbappe amepewa nguvu ya kweli kufuatia uamuzi wake wa kukataa dili la Real Madrid na kusalia PSG na inadhaniwa kuwa kutakuwa na mishe mishe kibao na klabu hiyo msimu unaokuja.
Na Neymar ni mmoja wa wachezaji kama hao ambaye anaweza kuwa mbioni kuondoka PSG. Mbrazil huyo alijiunga na PSG msimu wa joto wa 2017, dirisha la usajili sawa na Mbappe, lakini wakati thamani ya Mfaransa huyo ikipanda tangu wakati, Neymar yeye ameonekana kudorora.
Staa huyu alitatizwa zaidi na majeraha na kushindwa kutoa mchengo kwa kiwango kile kilichotarajiwa klabuni hapo.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.