Klopp Meneja Bora wa EPL Msimu wa 2021/22.

 

Jurgen Klopp ameshinda tena taji lingine msimu huu. Kocha huyo wa Liverpool alitunukiwa Tuzo ya Sir Alex Ferguson ya Meneja Bora wa Mwaka wa LMA.

Liverpool walipambana dhidi ya Manchester City hadi mechi ya mwisho katika mbio za kuwania taji la Ligi Kuu ya England ingawa walimaliza nafasi ya pili Klopp amefanikiwa kutwaa tuzo hiyo.

 

Kocha huyo wa Ujerumani alipokea tuzo hiyo kutokana na msimu bora na timu yake katika Ligi Kuu ya Uingereza, baada ya kubeba Kombe la Carabao na Kombe la FA na kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Klopp alizungumzia furaha yake kwa kushinda tuzo hiyo inayobeba jina la Sir Alex Ferguson.

“Ni heshima kubwa na ulikuwa msimu wa kusisimua,” Klopp alisema.

 

“Siku ya mwisho ya mechi ambapo mechi mbili pekee hazikuwa na maana, lakini nyingine, zote tulicheza kwaajili ya kitu.

 

“Kulikuwa hali ya wasiwasi kidogo, hayakuwa matokeo bora kwetu, lakini tayari tumeimaliza.

 

“Na unaposhinda tuzo kama hii wewe ni genius, au una timu bora zaidi ya makocha duniani – niko hapa na wakufunzi wangu wanne, na wanajua ni kiasi gani ninawathamini.” aliongeza.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe