Droo ya Kombe la Dunia Kufanyika Leo Qatar

Mchaka mchaka wa kuelekea Qatar unafikia katika hatua ya mwisho kinachobaki ni nani atacheza na nani kwenye hatua ya makundi kwa timu zilizofuzu kwa michuano hiyo.

Ijumaa ya tarehe 1 mwezi Aprili inafanyika droo rasmi ya michuano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar ambayo ndiyo wenyeji wa michuano hiyo katika Kituo cha Maonyesho na Mikutano cha Doha (DECC) Sherehe hizo zitahudhuriwa na wageni waalikwa 2,000.

Timu 29 kati ya 32 tayari zimefuzu wakiwemo wenyeji Qatar, Kutoka Ulaya, mabingwa wa zamani Ujerumani, Uhispania, Uingereza na Ufaransa tayari wameshakata tiketi zao za kwenda Qatar pamoja na Uholanzi, Croatia, Poland, Portugal, Serbia, Uswisi na Ubelgiji.

Kutoka Amerika Kusini  Brazil na Argentina tayari wamekata kibali cha kwenda Uarabuni pamoja na Ecuador na Uruguay.

Kutoka Asia, Iran na Korea Kusini pia watakuwa wakielekea Qatar bila kuwa sahau Saudi Arabia na Japan.

Afrika itawakilishwa na Cameroon, Ghana, Morocco, Senegal na Tunisia.

Amerika ya Kaskazini ina mataifa matatu Canada, Mexico na USA.

Hivi ndiyo timu zimewekwa kuelekea droo inayofanyika siku ya leo

Pot 1: Qatar, Brazil, Belgium, France, Argentina, England, Spain, Portugal.

Pot 2: Mexico, Netherlands, Denmark, Germany, Uruguay, Switzerland, USA, Croatia.

Pot 3: Senegal, Iran, Japan, Morocco, Serbia, Poland, South Korea, Tunisia.

Pot 4: Cameroon, Canada, Ecuador, Saudi Arabia, Ghana, Wales/Scotland/Ukraine, Costa Rica/New Zealand, Peru/UAE/Australia.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe